May 14, 2014



Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic ‘Loga’, ameukataa usajili wa mshambuliaji wa Mbeya  City, Saad Kipanga, ambaye amekuwa akielezwa kuwa anawindwa na timu hiyo.


Awali, viongozi wa klabu hiyo walifanya mazungumzo na mchezaji huyo ambaye alionyesha kiwango cha juu msimu uliopita ili kupata saini yake ambapo sasa zoezi hilo limesitishwa kufuatia sakata la uchaguzi linaloikabili klabu hiyo.

Kupitia chanzo  Loga ameiacha, hajaorodhesha jina la Kipanga.
“Kwa sasa usajili wa mchezaji huyo umekufa kutokana na suala la kutafuta viongozi wapya watakaoongoza timu yetu.
 “Inawezekana Kipanga akasajiliwa au kutosajiliwa kwa sababu Loga aliandika majina ya wachezaji ambao anawahitaji kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi cha kwanza ili kufanya vizuri msimu ujao.

“Lakini ukweli jina la mshambuliaji huyo sijaliona labda kama viongozi watafanya jeuri,” kilisema chanzo hicho. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic