Benchi la ufundi la Mbeya City
limehamishia makazi yake vijijini mkoani humo kusaka vipaji kwa ajili ya
kuimarisha kikosi chao kwa hofu ya
kukimbiwa na baadhi ya nyota msimu ujao.
Ofisa habari wa timu hiyo, Freddy
Jackson amesema wao ni sawa na Arsene Wenger
(kocha wa Arsenal ya England) kutokana na falsafa ya kuibua vipaji kabla ya
kuwa mastaa bora.
Jackson, aliongeza kuwa, tayari makocha
hao wamezamia vijijini kwa ndani kuangalia mechi za ‘ndondo’ ambapo wanaamini
wanaweza kupata vipaji vipya.
“Falsafa yetu ni sawa na Arsene Wenger, tunatafuta vipaji na
kuviendeleza hadi wanakuwa mastaa. Ndiyo maana makocha tayari wapo mitaani,
kule Ileje, Mwakalenge na kwingine kufuatilia ndondo ili waangalie anayewafaa,”
alisema Jackson.
Aliongeza kuwa kutokana na falsafa yao,
hawana muda wa kuhangaika na wachezaji wa timu kubwa, huku akikana tetesi za
kumtaka Uhuru Selemani wa Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment