MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI YA SIMBA, DAMAS NDUMBARO ALIPOKUWA MAKAO MAKUU YA FIFA MJINI ZURICH, USWISS |
Kamati ya Uchaguzi ya Simba imesema imepokea
taarifa zisizo rasmi za kuwepo watu wanaotengeneza orodha bandia za kulipia ada
ya uanachama wa klabu hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati
ya Uchaguzi ya Simba, Damasi Ndumbaro, ambaye kitaaluma ni mwanasheria.
Ndumbaro
alisema tunatoa onyo kali kwa wahusika wanaotengeneza orodha hizo feki ili
wapate nafasi ya kuingia kwenye uchaguzi na kupiga kura.
Ndumbaro amewataka wanachama wote wa klabu
hiyo kuhakikisha wanalipia ada zao za uanachama kwenye makao makuu ya Msimbazi
yaliyopo jijini Dar es Salaam na katika akaunti maalum inayojulikana.
“Jambo la kushukuru ni kwamba, uchaguzi utafanyika
kwenye Bwawo la Polisi, ninaamini ni sehemu nzuri yenye usalama kwa ajili ya
kupambana na wale watakaotaka kuingia kwenye mkutano kwa orodha feki.
“Kama kamati, mtu yeyote tutakayembaini
alikuwa ana orodha feki, basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa siku hiyo ya
uchaguzi,” alisema Ndumbaro.
0 COMMENTS:
Post a Comment