Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi wa Yanga, Alex Mgongolwa amesema wanachosubiri ni
kupitishwa kwa rasimu ya katiba.
Mgongolwa
amesema baada ya kupitishwa kwa rasimu ya katiba ndiyo kazi ya maandalizi ya
uchaguzi yataanza.
“Matumaini
yangu uchaguzi utafanyika mwanzoni mwa mwezi wa sita.
“Lakini sasa
hatuwezi kufanya lolotea hadi hapo rasimu ya katiba itakapopitishwa kwa
msajili.
“Tuna
matumaini mambo hayo yatakwenda vizuri katika kipindi mwafaka,” alisema
Mgongolwa.
Uchaguzi wa
Yanga unasubiriwa kwa hamu hasa baada ya mwenyekiti wake, Yusuf Manji kueleza
hadharani kuwa hatagombea.
0 COMMENTS:
Post a Comment