Kampuni ya ndege ya Etihad wameamua kufanya kufuru
kwa kuweka rekodi katika VIP yao.
VIP yao mpya inaonekana kama sawa na hoteli za
kitalii na wateja wataweza kulala kama wako hotelini.
Ndege hiyo ambayo ndiyo wadhamini wakuu wa Man City
ya England, watatumia ndege aina mbili ambazo ndiyo kubwa kuliko zote duniani.
Ndege ya kwanza ni Airbus A380 na Boeing B787
Dreamliner ambazo ndiyo ndege kubwa zaidi kuliko zote.
Kampuni hiyo makao makuu yake ni Abu Dhabi na ina
ushindani na ile ya Emirates inayoidhamini Arsenal na zote zikiwa zinatokea
Falme za Kiarabu maarufu kama UAE.
0 COMMENTS:
Post a Comment