Ikiwa zimepita wiki chache tangu Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA)
kilipomteua Shaban Ramadhani kuwa Kocha Mkuu wa Zanzibar Heroes, chama hicho
kimetengeua uamuzi wake huo na kumpa jukumu hilo, Ahmed Morocco ambaye aliwahi
kuwa kocha wa Coastal Union ya Tanga.
Uteuzi wa kocha wa Zanzibar Heroes unaonekana kama filamu kutokana
na maamuzi ambayo yanaonekana kama wahusika wanigiza, ambapo sababu za
Ramadhani kupokwa cho hicho inadaiwa ni kutokuwa na uhusiano mzuri na mmoja
wasaidizi wake ambaop alipangiwa kufanya nao kazi, huku yeye akikataa.
Katibu wa ZFA, Kassim Salum amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya
kuona kuwa Morocco ndiyo mwalimu pekee anayefaa kukinoa kikosi hicho kwa sasa
kutokana na uwezo mkubwa alionao.
“Kwa sasa kocha mkuu ni Morocco, tumezingatia vitu vingi mpaka
tukaamua kumpa wadhifa huo, kwanza yeye ndiye mwenye CV nzuri na ya juu kwa
makocha wa Zanzibar pia ana uzoefu mkubwa na timu yetu ya taifa,” alisema
Salum.
Kwa upande wake, Morocco alisema: “Ni kitu kizuri kuteuliwa kuwa
mwalimu wa timu kama hii, nafikiri wameuona uwezo wangu na kujua faida niliyo
nayo nikiwa kama kocha, kikubwa ni ushirikiano kwa kweli ili tufikie
tunapopataka na sasa nasubiri siku ya kuanza kazi rasmi, nianze majukumu yangu,”
alisema Morocco.
Inaelezwa kuwa
Ramadhani licha ya kuteuliwa tangu wiki kadhaa zilizopita, hakufanikiwa
kuiongoza timu hiyo katika mechi hata moja. Mpaka gazeti hili linaingia
mitamboni, hakupatikana kuzungumza kilitokea kwa upande wake.
SOURCE: CHAMPIONI JUMAMOSI
SOURCE: CHAMPIONI JUMAMOSI
0 COMMENTS:
Post a Comment