Ingawa mechi ni ngumu na wachezaji gumzo zaidi katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hivi punde ni Cristiano Ronaldo na wengine, lakini Real Madrid wanapaswa kuwachunga wachezaji wawili wa Atletico Madrid, maana wana uwezo na wanang'ara zaidi katika mechi ngumu.
TURAN:
Arda
Turan amezaliwa Januari 30, 1987, amewahi kuwa nahodha wa Galatasaray
akiwa na miaka 21 katika msimu wa 2009-10.
Ana uzoefu mkubwa na michuano ya
kimataifa, anajulikana kwa uwezo mkubwa wa kumiliki na kukimbia na mpira.
Lakini ujanja na mbinu za juu za
kubadilisha mchezo, pasi za mwisho na amekuwa akimlisha sana Diego Costa au
anayekaa namba tisa kufanya kazi ya ufungaji.
Lakini Turan ana uwezo mkubwa wa
kufunga mabao haraka na inaonyesha ni mzoefu kwa kuwa tayari ameichezea timu ya
taifa ya Uturuki mechi 71 na kufunga mabao 14.
Arda Turan ni mchezaji wa
kwanza mzaliwa wa Uturuki kushinda Kombe la La Liga baada ya Atletico kuwapiga
kumbo Barcelona na Real Madrid msimu wa 2013-2014 na kulibeba.
KOKE:
Jina lake halisi ni Jorge Resurrección
Merodio, mashabiki
wanamuita Koke, kinda tu maana
amezaliwa Januari 8, 1992, lakini ni ‘mbaya’.
Anajulikana kwa uwezo mkubwa wa kuanzisha
mashambulizi, pasi za mwisho na krosi za maana.
Lakini ukizubaa, anafunga na hadi leo
Barcelona hawajamsahau kwa kuwa ndiye alifunga bao lililowatoa na kuipeleka
Atletico Madrid fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Amezaliwa Madrid, ametua Atletico akiwa na
miaka 9, hivyo si mgeni na anajua timu yake inataka nini hivi punde.
0 COMMENTS:
Post a Comment