Matibabu ya Yaya Toure nchini Qatar
yaliyokuwa yakifanyika kwa siri bila kuelezwa tatizo ni nini, imegundulika ni
nyama za paja.
Yaya amefunga safari hadi nchini Qatar
kupata matibabu wakati kikosi cha Ivory Coast kikiwa jijini Florida, Marekani kujiandaa na Kombe la Dunia
litakalopigwa nchini Brazil.
Imeelezwa hadi Alhamisi, Yaya atajiunga na
wenzake, lakini tayari kuna ushauri umetolewa na daktari asicheze mechi ya
kwanza ili kupata muda mzuri wa kupumzika.
KOCHA WA IVORY COAST, SABRI LAMOUCHI AKIWA NA SALEH ALLY MARA BAADA YA MAHOJIANO HIVI KARIBUNI. |
Kocha Mkuu wa Ivory Coast, Sabri Lamouchi
amethibitisha kuhusiana na Toure ambaye aliumia mechi nne kabla ya kwisha kwa
Ligi Kuu England lakini akarejea uwanjani.
0 COMMENTS:
Post a Comment