ULIMWENGU |
Washambuliaji wawili, Thomas Ulimwengu
na Mbwana Samatta hawatakuwepo nchini kuitumikia Taifa Stars itakapoivaa
Zimbabwe.
Stars itapambana na Zimbambwe Mei 17 au 18 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam katika mechi ya kuwania ku[ata nafasi ya makundi kupigania nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa Afrika.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa Samatta na Ulimwengu watakuwa na majukumu ya michuano ya kimataifa katika kikosi chao cha TP Mazembe.
“Kweli hawatakuja na ufafanuzi uko hivi,
Caf wamezipanga mechi hizi za mtoano katika kipindi ambacho ni nje ya kalenda
ya Fifa.
“Hivyo bado klabu zinakuwa na haki na
wachezaji, tukifanikiwa kuingia katika hatua za makundi, hizo zinatambulika na
kalenda ya Fifa.
“Hivyo sasa klabu zinakuwa na haki na
wachezaji kuliko shirikisho na hatuna namna kwa kuwa wao wanasema wanawahitaji,”
alisema Msemaji wa TFF, Boniface Wambura ambaye ni mmoja wa waandishi
waandamizi wa michezo.
0 COMMENTS:
Post a Comment