Shirikisho
la Mpira wa Soka Afrika (Caf) limeteua waamuzi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Kongo (DRC) kuchezesha mechi kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na
Nigeria.
Mechi
ya mchujo kusaka tiketi ya kucheza Fainali za 19 za Afrika kwa vijana wenye
umri chini ya miaka 20 zitakazofanyika mwakani nchini Senegal itachezwa
wikiendi hii jijini Dar es Salaam.
Waamuzi
hao wataongozwa na Jean-Jacques Ndala Ngambo atakayesaidiwa na Oliver Safari Kabene,
Nabina Blaise Sebutu na Mupemba Ignace Nkongolo. Kamishna wa mechi hiyo namba
37 ni Poiret Antoine Ralph Danny kutoka Shelisheli.
0 COMMENTS:
Post a Comment