Rybolovlev akiwa na bintiye, Anna. |
*Fedha walizotoa
Chelsea kumpata Torres, yeye alimnunulia bintiye nyumba
*Akanunua nyumba
ya Will Smith na sasa anamiliki kisiwa nchini Ugiriki
MONACO, Ufaransa
MAISHA kila siku
yana mambo mapya, kwani mahakama ya nchini Switzerland imemuamuru bilionea wa
Kirusi, Dmitry Rybolovlev, 47, kumlipa aliyekuwa mkewe pauni bilioni 2.6 (zaidi
ya Sh trilioni 7.2).
Rybolovlev
ametakiwa kumlipa Elena Rybolovlev, kiasi hicho ambacho kinaaminika kufikia
nusu ya utajiri wake na mahakama imeona itakuwa ni sahihi kwa kuwa wawili hao
waliishi kwa miaka 24 kabla ya kutengana baada ya kulumbana kwa kipindi.
Baada ya
kutengana mwaka 2008, Elena aliamua kufungua kesi hiyo ambayo imekuwa
ikiunguruma bila ya kupata jibu hadi uamuzi huo ulipotolewa.
Rybolovlev ndiye
mmiliki wa Klabu ya AS Monaco ya Ufaransa ambaye aliwanunua wachezaji maarufu
kama Radamel Falcao akitokea Atletico Madrid na baadaye mshambuliaji wa zamani
wa Manchester United, Dimitar Berbatov.
JUMA ANALOMILIKI MAREKANI |
Kama Rybolovlev
atakubali kutoa kiasi hicho cha fedha, itakuwa ni rekodi ya talaka ghali zaidi
kutolewa duniani kutokana na malipo hayo.
Fedha
atakayomlipa Rybolovlev inaweza kuinunua klabu yoyote kubwa duniani kwa kuwa
hata AS Monaco aliinunua kwa kiasi ambacho hakifikii fedha hiyo.
Talaka zilizokuwa
ghali zaidi awali na malipo yake kuonekana ni juu ni ile aliyotoa Alec
Wildenstein kwa aliyekuwa mkewe, Jocelyne. Alimlipa pauni milioni 1.5 (zaidi ya
Sh bilioni 4). Kabla ya hapo Rupert Murdoch, bilionea wa mambo ya habari,
alimlipa aliyekuwa mkewe Anna, kitita cha pauni bilioni moja (Sh trilioni 2.9),
hiyo ilikuwa mwaka 1999.
Keshi ya
Rybolovlev iliendeshwa kwa kipindi cha miaka sita bila ya mafanikio lakini sasa
bilionea huyo aliyepata mafanikio kupitia masuala ya kilimo, analazimika
kugawana mali zake na mkewe huyo.
Tayari mkewe huyo
amedai kupewa moja ya mali ghali za Rybolovlev kwa kuwa ametaka apewe kisiwa kilicho
nchini Ugiriki anachomiliki mumewe, chenye thamani ya pauni milioni 100 (zaidi
ya Sh bilioni 278) pamoja na jumba moja la kifahari lililopo nchini Marekani.
Mwanamama huyo
ambaye ana mtoto mmoja aliyezaa na Rybolovlev aitwaye Anna, 13, anaishi nchini
Uswiss na ametaka malipo yake yote kufanyika nchini humo huku akisisitiza
kubaki na jumba la kifahari analoishi nchini humo.
Utajiri wa Rybolovlev
unakadiriwa kufikia pauni bilioni 5.2 (zaidi ya Sh trilioni 14).
Uhamisho wa
Torres:
Rybolovlev ni
bilionea kweli, pamoja na umiliki wa Klabu ya AS Monaco, lakini mwaka 2012
alinunua nyumba ya pauni milioni 50 (Sh bilioni 139) ambazo ni sawa na uhamisho
gumzo wa Fernando Torres kutoka Liverpool kwenda Chelsea na ndiyo ghali kwenye
Ligi Kuu England.
Lakini fedha hizo
zote alitoa kumnunulia nyumba binti yake Anna ambaye alikuwa amehamia New York,
Marekani kwa ajili ya kusoma chuo kikuu. Rybolovlev anamiliki majumba mengine
ya kifahari lakini hiyo aliinunua katikati ya mji ili binti yake huyo awahi
kufika shule.
Pamoja na
kuimiliki AS Monaco, anamiliki kitita cha pauni milioni 295 katika benki ya Cyprus.
Pia ana jumba la ufukweni kule Palm Beach, Florida lenye thamani ya dola
milioni 95 ambalo alilinunua kwa milionea mwingine, Donald Trump.
Rybolovlev aliendelea
kuonyesha jeuri ya fedha baada ya kutoa pauni milioni 12 na kununua nyumba
iliyokuwa inamilikiwa na msanii maarufu wa filamu na muziki wa Marekani, Will
Smith.
Kuonyesha bado
fedha ‘inatema’, Rybolovlev akatoa pauni milioni 178 na kununua jumba la
kifahari katika eneo la La Belle Epoque mjini Monaco na ndiko amekuwa akiishi.
AS Monaco:
Desemba, 2011,
kama utani vile alitangaza kuinunua Klabu ya AS Monaco, lengo lilikuwa ni
kuifanya bora ikiwezekana kuizidi PSG ambayo inamilikiwa na bilionea wa Kiarabu
kutoka Qatar.
Rybolovlev anamiliki
mali kadhaa nchini Ufaransa ambazo zinaelezwa kuzidi pauni milioni 100.
Ujeuri:
Rybolovlev
anaaminika ni kati ya watu wajeuri sana, kwani mkewe Elena tangu ametengana
naye, amekuwa akifuatiliwa na wapelelezi binafsi usiku na mchana.
Wakati fulani Elena
alihojiwa na polisi wa Cyprus kwa madai aliiba pete yenye vito vya madini ya
almasi aliyoazima kwa bintiye Anna lakini hakuirudisha. Hata hivyo aliachiwa
bila ya kufunguliwa mashtaka.
Jela:
Elena aliwahi
kuishi jela miezi 11 akiwa na mumewe kutokana na kashfa ya kudaiwa kumuua
mpinzani wake kibiashara.
Hata hivyo,
mwisho Rybolovlev alishinda kesi hiyo na wote wakarejea uraiani na kuendelea na
maisha ya kawaida.
Lakini Rybolovlev
amekuwa akitembea akiwa amevaa koti lisilopitisha risasi akionyesha kuwa
anahofia usalama wake. Wakati fulani alilazimika kuihamishia familia yake
nchini Switzerland kutokana na kuhofia usalama wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment