Uongozi wa JKT Ruvu na kocha wake, Fred Minziro, bado wapo katika
mvutano wa kuingia mkataba mpya kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao
ikiwa ni sababu za kimaslahi.
Minziro alitua JKT kwa ajili ya kuisaidia timu hiyo kufuatia kuwa
katika mwenendo mbaya wa ligi na hatimaye kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya
nane.
Katibu wa JKT, David Ngaga amesema kuna baadhi ya vitu ambavyo hawajakamilishana na Minziro, ndiyo
maana bado hawajaingia naye mkataba.
“Bado tupo katika mazungumzo na Minziro na iwapo tutamalizana,
basi tutaingia naye mkataba mpya.
“Kuna kitu kimoja bado hatujafikia muafaka, hivyo mambo yakiwa
sawa atakuwa kocha wetu msimu ujao,” alisema Ngaga.
Aidha kwa upande wa Minziro alifunguka kuwa bado hajasaini mkataba
na anausubiri uongozi wa timu hiyo ili uweze kufikia makubaliano ya kuingia
mkataba mpya ikiwa ni pamoja na kufanya usajili.
0 COMMENTS:
Post a Comment