Kiungo
mshambuliaji wa timu ya Al Markhiya ya Qatar, Mwinyi Kazimoto amewasili nchini
kujiunga na kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na mechi ya michuano ya
Afrika dhidi ya Zimbabwe.
Kazimoto
ambaye amewasili nchini jana (Mei 5 mwaka huu) anatarajia kusafiri leo (Mei 6
mwaka huu) kwenda Tukuyu mkoani Mbeya ambapo Taifa Stars imeweka kambi yake
chini ya Kocha Mart Nooij kujiandaa kwa mechi hiyo.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager juzi (Mei 4 mwaka huu)
ilicheza mechi ya kirafiki na Malawi (Flames) ikiwa ni sehemu ya maandalizi
kabla ya kuikabili Zimbabwe (Mighty Warriors). Mechi hiyo dhidi ya Flames
ilichezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine na kumalizika kwa suluhu.
0 COMMENTS:
Post a Comment