Kamati ya uchaguzi ya Simba imefanya kazi ya
kuwahoji wagombea na walioweka pingamizi chini ya ulinzi mkali.
Waandishi wa habari na watu wengine walizuliwa
kuingia katika eneo la Gymkhana jiji Dar es Salaam kusaidia kufanyika kwa zoezi
hilo kwa utulivu.
Askari waliokuwa getini waliuia kila mtu
kuingia katika eneo hilo isipokuwa wanachama wa klabu hiyo ya Gymkhana,
wagombea na walioweka mapingamizi.
Lakini kamati imefanya kazi hiyo ya kuwahoji na
imeelezwa kuwa kesho itamalizia kazi hiyo.
“Kesho Jumanne, kamati ndiyo itatoa majibu,
lakini kila mtu kahojiwa leo.
“Kutakuwa na mambo fulani ya kupitia halafu
baada ya hapo, mwenyekiti Dokta Damas Ndumbaro atatangaza,” kilieleza chanzo.
Taarifa zinasema kamati hiyo haijamaliza baadhi
ya mambo hivyo inalazimika kuendelea na zoezi kesho.
0 COMMENTS:
Post a Comment