MASHALI MWENYE KOFIA NA RASTA, AKIMTUPIA KONDE MAUGO MWENYE SHATI YA MISTARI. |
Mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali usiku wa kuamkia jana (Jumapili)
walitibua hali ya hewa baada ya kutwangana nje ya ulingo wakati wakisubilia
pambano la mabondia wenzao, Karama Nyilawila na Said Mbelwa waliokuwa
wakigombea mkanda wa ubingwa wa UBO katika Ukumbi wa Friends Corner Manzese
jijini Dar es Salaam.
Katika tukio Mashali kwa muda mrefu alionekana akikata kilaji na bondia
mwenzake, Francis Miyeyuso 'Chichi mawe' aliyekuwa na mkewe lakini baada ya
muda aliwaacha na kwenda kukaa karibu na Maugo. Muda si mrefu Mashali
alionekana kubwatizana na Maugo ambapo wote walisimama na kuvaana hali
iliyosababisha vurumai na viti kurushwa hovyo lakini baada ya muda waliamuliwa.
Baada ya sakata hilo kutulia Championi Ijumaa lilizungumza na Maugo
ambaye alisema ameshangazwa na ugomvi huo ambao inaonekana Mashali aliupanga.
"Yaani mimi namshaangaa huyu, mimi nimejikalia zangu hapa sijui
amekula miunga yake na mipombe anakuja kuntukania mama yangu, hivi anamjua mama
yangu huyu," alisema Maugo huku akiporomosha matusi ya nguoni.
Gazeti hili lilizungumza na Mashali kuhusiana varangati hilo ambapo
bondia huyo aliendelea kumwaga matusi mazito kwa mwenzake.
"Hana lolote nimeshamdunda mara mbili ulingoni, kwanza Diamond
Jubilee na mara nyingine pale PTA Sabasaba lakini hataki kuniheshimu, wangeacha
na leo nimfunze tena adabu nje ya ulingo," alisema Mashali huku pia
akiporomosha maneno makali.
0 COMMENTS:
Post a Comment