Na
Saleh Ally
REAL
na Atletico Madrid zilivuka katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa
zikionyesha zilikuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ulaya.
Wababe
hao wa mji wa Madrid wanakutana leo jijini Lisbon, Ureno katika fainali
itakayoamua ipi klabu bora zaidi kisoka barani Ulaya.
Hakuna
aliyekuwa akiipa nafasi Atletico Madrid kuwa itafikia fainali, lakini dalili
zilianza kuonekana baada ya mechi sita za kundi G.
Atletico
dhidi ya Diego Simeone, baada ya mechi 6 za kundi G ilimaliza ikiwa kinara na
pointi 16 na ndizo pointi ilizopata Real Madrid ikiwa katika kundi B.
Kingine
ambacho kinaonyesha mechi ya leo itakuwa na ushindani mkubwa ni namna takwimu
za wakati wa makundi zinavyofanana kwa timu hizo mbili.
Achana
na pointi 16, lakini Real Madrid ilishinda mechi 5 kati ya 6, ikatoka sare moja
tu na ndicho kimetokea kwa Atletico Madrid katika kundi G.
Ukiachana
na kufanana kwa pointi, michezo ya ushindi na sare, kulikuwa na tofauti kwenye
mabao ya kufunga na kufungwa na kila upande ukionyesha sifa tofauti.
Real
Madrid imefunga mabao mengi zaidi wakati wa hatua ya makundi, ilipachika 20 na
Atletico ikafikisha 15, maana yake Madrid ina safu kali ya ushambuliaji.
Lakini
kwenye ulinzi, Madrid ikaruhusu mabao 15 na Atletico ikaruhusu 12, hii
inaonyesha vijana wa Simeone ni bora kwenye ulinzi zaidi ya wale wa Carlo
Ancelott.
Katika
kundi B, Madrid ilikuwa na timu za Galatasaray, Juventus na Copenhagen wakati
ndani ya Kundi G, Atletico ilipambana na Zenit, FC Porto na Austria Wien.
Kuanzia
hatua za makundi kwa takwimu, inaonekana Madrid na watani wao wa jadi Atletico
ni timu zisizopishana viwango kwa kiasi kikubwa.
Hii
ni sehemu ya kuonyesha fainali hiyo ni ngumu na haina mwenyewe, maana yake timu
yoyote inaweza kuwa bingwa leo.
Timu
nyingine kutoka katika makundi ambazo zilipiga hatua kubwa ni kutoka kundi D na
H.
Barcelona
iliingia nusu fainali ikitokea kundi H na Bayern ndiyo walikuwa vinara wa kundi
D.
Lakini
mwisho, Barcelona wakakiona cha moto kutoka kwa Atletico na mabingwa watetezi,
Bayern, wakavuliwa kombe kwa aibu dhidi ya Madrid.
Makocha
wote wawili wamewahi kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiwa wachezaji,
Ancelott na AC Milan na Simeone na Inter Milan, zote za Italia.
Lakini
Ancelott akalichukua akiwa na AC Milan, sasa huenda ikawa ni zamu ya Simeone
ambaye akifanya hivyo, atavunja ndoto ya Madrid kutwaa Kombe la 10 la Ligi ya
Mabingwa.
|
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GF
|
GA
|
GD
|
Pts
|
1
|
6
|
5
|
1
|
0
|
20
|
5
|
15
|
16
|
|
2
|
6
|
2
|
1
|
3
|
8
|
14
|
-6
|
7
|
|
3
|
6
|
1
|
3
|
2
|
9
|
9
|
0
|
6
|
|
4
|
6
|
1
|
1
|
4
|
4
|
13
|
-9
|
4
|
|
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GF
|
GA
|
GD
|
Pts
|
1
|
6
|
5
|
1
|
0
|
15
|
3
|
12
|
16
|
|
2
|
6
|
1
|
3
|
2
|
5
|
9
|
-4
|
6
|
|
3
|
6
|
1
|
2
|
3
|
4
|
7
|
-3
|
5
|
|
4
|
6
|
1
|
2
|
3
|
5
|
10
|
-5
|
5
|
0 COMMENTS:
Post a Comment