Baada ya Taifa Stars kushindwa kuonyesha cheche
katika mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi jijini Mbeya, ngoma inarudiwa Jumanne (Mei 27).
Taarifa kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) zinaeleza Malawi wanatua nchini kesho au keshokutwa kuivaa Taifa Stars
chini ya Mart Nooij.
Mechi yake ya kwanza akiwa na Stars, Nooij aliivaa
Malawi mjini Mbeya na mechi ikaisha kwa sare.
Sasa anaivaa Malawi kwa mara ya pili ikiwa ni mechi
yake ya tatu baada ya ile ya pili kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe.
TFF imeamua kuiandalia Stars mechi hiyo dhidi ya
Malawi kabla ya kwenda kuivaa Zimbabwe katika mechi ya marudiano jijini Harare.
Malawi inaaminika kucheza katika mtindo wanaoutumia
Zimbabwe na ndiyo moja ya timu zimekuwa zikiisumbua sana Zimbabwe kila
zinapokutana.
Baada ya mechi dhidi ya Malawi, Stars itakuwa
tayari kuanza safari kwenda Harare kupambana.
0 COMMENTS:
Post a Comment