June 18, 2014



Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Kassim Dewji, ameibuka na kusema kuwa usajili wa klabu hiyo msimu ujao utatisha kutokana na mchakato waliouandaa kwa ajili ya kuboresha kikosi hicho.


Simba inatarajiwa kufanya uchaguzi wake mkuu Juni 29, baada ya viongozi waliokuwepo madarakani kumaliza muda wao wa miaka minne.

Dewji amesema kuwa wanafanya usajili kimyakimya na wanatarajia kuwa na usajili uliokwenda shule na kudai kuwa lengo lao kubwa ni kutwaa ubingwa msimu ujao.

“Tunapata viongozi wapya Juni 29, hivyo tunatarajia kuwa na timu bora yenye ushindani, usajili utakuwa mzuri na tunatarajia kupata wachezaji wazuri mara baada ya mchakato wa uchaguzi kukamilika.

“Tunasubiri viongozi wapya ili mchakato uanze kwani msimu ujao lazima tutwae ubingwa wa ligi.

“Siwezi kusema ni wachezaji gani tutawasajili, uchaguzi ukimalizika  itajulikana ni akina nani watasajiliwa na tutawaweka hadharani,” alisema Dewji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic