June 18, 2014


NINYONZIMA (KULIA) AKIWA NA WACHEZAJI WENZAKE WA YANGA.


Kiungo mchezeshaji wa Yanga Mrwanda, Haruna Niyonzima, ameitaka kamati ya usajili ya timu hiyo chini ya mwenyekiti wake Abdallah Bin Kleb, kuhakikisha inamsajili mshambuliaji mwenye uwezo wa kupachika mabao.


Timu hiyo hadi hivi sasa tayari imefanikiwa kuwasajili wachezaji wawili pekee ambao ni kiungo mkabaji, Said Juma na beki wa pembeni, Saleh Abdallah.

Niyonzima amesema kuwa safu ya ushambuliaji inatakiwa iwe ya kwanza kufanyiwa marekebisho kwa kumsajili mshambuliaji namba tisa ambaye yeye kazi yake ni kufunga peke yake.

Niyonzima alisema safu hiyo ya ushambuliaji ndiyo iliyosababisha timu yao ishindwe kufanya vizuri  kuanzia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika (Caf) na Ligi Kuu Bara.

“Nikisema kuwa Yanga isajili mshambuliaji, siyo kwamba waliopo hawana uwezo kabisa, hapana wana uwezo mkubwa isipokuwa anahitajika mwingine kwa ajili ya kuiongezea nguvu nafasi hiyo.

“Ninaamini kuwa wapo washambuliaji wengi wenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao, hivyo ninaiomba kamati husika kuhakikisha inampata mshambuliaji wa aina hiyo,”alisema Niyonzima.
Nafasi hiyo ya ushambuliaji kwenye msimu uliopita wa ligi kuu ilikuwa ikichezwa na Jerry Tegete, Shabani Kondo, Said Bahanuzi, Hamis Kiiza, Emmanuel Okwi, Mrisho Ngassa na Didier Kavumbagu aliyetimkia Azam FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic