June 14, 2014




Watumiaji wa simu za kisasa za Smart Phone wametakiwa kutumia chaji za Puku kuchajia simu zao ili kujihakikishia usalama wake.


Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa chaji hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUKU alisema kuwa chaji hizo kwa sasa zinapatikana hapa nchini.


Alisema kuwa ni chaji ambazo zinahifadhi umeme kwa muda mrefu ambao unakuja kutumiwa kuchajia simu hasa pale ambapo panakuwa hakuna umeme.

Aliongeza kuwa bei yake kwa sasa ni kuanzia 160,000 kutokana na ubora wake na pamoja na namna ambavyo inasaidia.
"Mimi ni mtanzania kutoka Tanga na nilisoma hapa hapa ila nilielekea Marekani kusoma na ninaishi huko na nimebuni hii chaji kwa lengo la kusaidia watu mbalimbali ambao wanakuwa wakisumbuliwa na tatizo la kuchajia simu zao pale ambapo panakuwa hakuna umeme wa uhakika"alisema Meck Mbwana ambaye ni mvumbuzi na mkurugenzi mtendaji wa PUKU.

Aliongeza kuwa " kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya simu za smart phone huku watumiaji wakilalama kuwa wanakosa uhakika wa umeme wa kuzihudumia sasa hii bidhaa itasaidia".

Aliongeza kuwa kwa sasa zinapatikana hapa nchini na aliwataja wahusika wakubwa kuwa ni pamoja na Ed Kavishe-mshirika mwenza, Joseph sikare – Rais Tanzania huku Mwanamitindo Millen Magese akiwa ni mshirika mwenza na balozi wao.
Kwa upande wake Millen aliwataka wananchi kutumia bidhaa hiyo kwa kuwa mbali na kuwa ni ubora bali pia ni bidhaa ya watanzania wenyewe.

Tayari PUKU wameshajikita na uchangiaji wa huduma kwa jamii ambapo asilimia kadhaa ya mauzo itaelekezwa kwenye kampeni ya uelewa wa hali ya endometriosis na ujenzi wa hospital kwa ajili ya magonjwa yanayowasumbua akina mama. Mbali na udhamini wa kampeni ya endometriosis PUKU watachangia ujenzi wa madarasa mawili yaliyoko chini ya mradi wa Millen Magese Foundation yanayojengwa huko Mtwara ambapo mpaka sasa madarasa matatu yameshakamilika.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic