Kocha mtarajiwa wa Yanga, Marcio Maximo ndiye atakuwa anapendekeza wachezaji
anawaowataka kwa ajili ya kuboresha kikosi chake.
Taarifa
zinaeleza, baada ya Maximo kuomba apewe nguvu ya mwisho kwenye usajili, Yanga
imekubali kumkabidhi.
Habari za
uhakika kutoka kwa upande wa wakala anayeshughulikia ujio wa Maximo zinaeleza
sasa atakuwa akipendekeza na kusajili wachezaji anaoamini watakisaidia kikosi
chake.
“Sasa
makubaliano ni asilimia zaidi ya 95, wakati wowote anakuja na tayari kocha
ameomba kupewa rungu la usajili na imekubalika,” alisema.
Maximo ndiye
kocha mtarajiwa kuziba pengo la Hans van der Pluijm, raia wa Uholanzi ambaye
ameondika baada ya kupata dau la juu.
Lakini imekuwa
ikielezwa wachezaji wa Yanga wamekuwa na hofu kuhusiana na ujio wake na hasa
Juma Kaseja na Athumani Iddi Chuji ambao wamekuwa hawaelewani.
Lakini
uongozi wa Yanga umesisitiza kuwa bado uko kwenye mazungumzo na kocha huyo na masuala
mengine yote yanawezekana.
0 COMMENTS:
Post a Comment