Cameroon
imeng’olewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia baada ya kuchapwa bao 1-0 na
Croatia.
Croatia
ndiyo nchi anayetotokea Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic ambayo ilianza
michuano hiyo kwa kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Brazil.
Cameroon
walionyesha kutokuwa makini, walipoteza nafasi nyingi za wazi na mwisho
wakaambulia kipigo hicho huku nahodha wao, Samuel Eto’o akiwa kwenye benchi
anashuhudia.
Kiungo
nyota, Alex Song naye akalambwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kiwiko
Mario Mandzukic ambaye anachezea Bayern Munich.
Lakini
kichekesho zaidi wachezaji wawili, kiungo Benoit Assou-Ekotto na beki Benjamin
Moukandjo walikunjana na nsura wazichape baada ya kulaumiana baada ya mechi
hiyo lakini wakaamulia.
Kipigo
hicho cha jana cha Cameroon ni cha nne kutoka kwa Croatia katika mara zote
ambazo wamewahi kukutana.
0 COMMENTS:
Post a Comment