June 19, 2014



Kujua Michael Wambura anaendelea au la katika uchaguzi wa Simba, itajulikana leo.
Kazi ya kuanza kusikiliza rufaa yake ni saa nane kamili mchana kwenye hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.


Wambura aliyeenguliwa kuwania urais Simba amewasilisha hoja tisa kupinga hilo, kamati ya uchaguzi imetupia hoja 12.
Maana yake kutakuwa na ugumu wa mambo ya huenda jambo hilo litachukua muda mwingi.

Awali kamati ya maadili ilimrejesha Wambura kwa kura za vidole baada ya mambo kuwa magumu kutokana na utetezi uliowasilishwa na kamati ya uchaguzi ya Simba.

Suala hilo lilizua mkanganyiko mkubwa na ikaonekana haikuwa sahihi. Lakini bado kamati hiyo ilitoa ufafanuzi, ambao pia bado uliendelea kuwagawanya walioamini sahihi na wengine wakapinga.

Safari hii, kamati hiyo imemtoa Wambura baada ya kumbaini alipiga kampeni kabla ya muda.

Wambura alifanya mkutano na waandishi wakati akipeleka rufaa kwa mbwembwe, halafu akafanya hivyo tena baada ya kushinda. Lakini safari hii, rufaa yake iliwasilishwa kimyakimya bila ya wapambe wala kelele na hakukuwa na mkutano wowote na waandishi, hali inayoonyesha amegundua kuna tatizo na ameamua kulifanyia kazi.


Kabla Wambura pamoja na mgombea mwingine wa urais, Evans Aveva walionywa kutokana na kupiga kampeni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic