Mfadhili wa zamani wa Simba, Azim Dewji amesema
alichokieleza kuhusiana na njama za TFF kutaka kumrudisha madarakani, Michael
Wambura kimekamilika.
Lakini akasisitiza, kukamilika kwake kumekuwa na
uwazi na kuonyesha hakukosea hata kidogo.
“Nani anaweza kupinga tena kwamba Wambura
amerudishwa kwa hila kama nilivyoeleza.
“Suala la sheria na upigaji kura linatokea wapi,
sheria inaamuliwa kwa vipengele.
“Ndiyo maana nilisema TFF ni kawaida yake
kufanya maamuzi ambayo yanaiumiza Simba, hii si mara ya kwanza.
“Wao waliofanya hivyo wanajua kuwa walichofanya
si sahihi, lengo ni urafiki na kusaidiana.
“Kwa nini kusaidiana kwa maslahi ya watu binafsi
badala ya kufuata sheria na kanuni ambazo ziko wazi.
“Sasa hakuna anayeweza kusema nilikuwa nafanya
fitna, nilichozungumza nilikuwa nakijua na watu wanielewe vizuri. Sasa imebaki
kidogo tu, TFF kuchagua nani awe Rais wa Simba,” alisema Dewji.
Wiki iliyopita, Dewji ambaye alichangia kwa
kiasi kikubwa Simba kufika fainali ya Kombe la Caf mwaka 1993, alisema kuwa
lazima kamati ya rufaa ya TFF itamrudisha Wambura kugombea nafasi ya urais
Simba baada ya kuwa amekatwa na kamati ya uchaguzi ya Simba.
Kweli, kamati hiyo imemrudisha Wambura kuwania
kiti cha urais, licha ya kwamba kamati ya uchaguzi ya Simba ilisema kuwa
uanachama wake una walakini.
0 COMMENTS:
Post a Comment