June 12, 2014

AKILIMALI AKIWA NA KIONGOZI WA VIJANA WA YANGA, BAKILI MAKELE.


Kiongozi wa Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali amesisitiza, kuna watu wanaolazimisha migogoro ndani ya Yanga kwa njaa zao.


Mzee Akilimali ameiambia SALEHJEMBE, kwamba kama alivyoeleza kwenye mkutano wa jana, wanaendelea kufuatilia wanaonzisha chokochoko.
“Kijana, hauwezi kuniambia wanachama wote waliokuwa kwenye mkutano ule hawajielewi.
“Hauwezi kusema sisi wazee na vijana wote hatujui tunalofanya, isipokuwa hao wachache ambao hawana lolote, ni njaa zao tu.
“Yanga si sehemu ya kutafuta shibe, timu inataka maendeleo na tunataka kuona inashinda kwa kuwa ndiyo furaha yetu,” alisema Akilimali huku akisisitiza.
“Tutawapata tu hao walioandikisha majina ya wanachama waliofariki dunia na kuyawasilisha TFF eti wanapinga uongozi wa Manji kuongezewa mwaka mmoja.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic