June 26, 2014



Mshambuliaji wa Liverpool na Uruguay, Luis Suarez atakaa nje ya uwanja kwa miezi minne.


Hiyo ni adhabu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ikiwa ni baada ya kumuuma beki Girgio Chiellini katika mechi ya hatua ya makundi Kombe la Dunia.
Pia limemfungia kucheza mechi tisa zilizo chini ya Fifa, maana yake anaondoka na hataichezea Uruguay katika Kombe la Dunia linaloendelea nchini Brazil na tayari timu hiyo imefuzu hatua ya 16 Bora.



Mwanasheria wa mshambuliaji huyo, Alejandro Balbi, alisafiri hadi Rio de Janeiro kumtetea mteja wake.

Balbi ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka la Uruguay alisema England na Italia imekuwa ikilikuza suala suala hilo na kuita ni “kampeni ya watu wa Ulaya kumuangamiza Suarez”.

Pamoja na adhabu hiyo kali, Suarez amepigwa faini ya kitita cha pauni 65,000 na Uruguay imepewa siku tatu za kukata rufaa.


Suarez alimuuma Chiellini ambaye hakuwa na mpira, kitu ambacho amekifanya mara ya tatu.
Kwa adhabu hiyo, Suarez kama atabaki Liverpool, ataanza kuichezea Oktoba wakati Ligi Kuu England itaanza Agosti.
Tukio la safari hii kumuuma beki, limetokea mara ya tatu kwa kuwa aliwahi kufanya hivyo wakati akiichezea Ajax ya Uholanzi, kabla ya kumuuma beki wa Chelsea, Blanislav Ivanovic.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic