Wanachama wa Simba juzi walifanya
maandamano ya kupinga maamuzi ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi, kusimamisha Uchaguzi Mkuu wa Simba lakini walifika mbali zaidi
kwa kutamka kuwa rais huyo ni mwanachama wa Yanga na anataka kuharibu mipango
yao.
Wanachama hao walifanya maandamano yao hayo
kwenye makao makuu ya timu hiyo, Kariakoo Msimbazi, Dar, wakiwa na kadi zao
mkononi huku wakizungumza hili na lile lakini kubwa ni kupinga maamuzi ya kiongozi
huyo.
Wanachama hao walisikika kwa pamoja
wakiimba wa hisia kwamba: “Huyo Malinzi kumbe Yanga, huyo Malinzi kumbe Yanga…
Tunataka uchaguzi, tunataka uchaguzi.”
Hata hivyo, mmoja wa wanachama anayetoka
Tawi la Mpira Pesa, Ras Simba, alitoa kauli ya kujitolea kutaka kumpa semina
rais huyo ya uongozi wa soka kwani anavyofanya sasa ni tofauti kabisa na
misingi ya uongozi.
“Nafikiri huyu bwana soka limemshinda na
hana misingi ya uendeshwaji wa mpira, mimi naelewa zaidi masuala ya soka, nampa
nafasi ya bure aje kwangu nimfundishe jinsi soka linayotakiwa kwenda.
“Haya mambo anaweza akachukulia ni ya
kawaida lakini anatakiwa kutambua kuwa soka linagusa hisia za ndani za watu
wengi kwa hiyo anatakiwa arekebishe maamuzi yake mapema,” alisema mwanachama
huyo mwenye kadi namba 05757.
0 COMMENTS:
Post a Comment