Wazee na
vijana wa Yanga wameanza uchunguzi wa kubaini majina ya wanachama waliofariki
dunia kutumika kupinga mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kuongezewa mwaka mmoja
wa uongozi na wanachama.
Wazee wa
Yanga wakiongozwa na Katibu wa Baraza hilo, Ibrahim Akilimali na Mwenyekiti wa
Baraza la Vijana, Bakili Makele, leo wametangaza kuanza uchunguzi huo.
Wamesema kuwa
wanataka kuwabaini wanachama waliojifanya wako 250 na kupeleka barua TFF
kupinga kitendo cha mwenyekiti wa Klabu hiyo kuongezwa mwaka mmoja
kuingoza klabu hiyo katika mkutano wa klabu hiyo wa maboresho ya katiba
uliofanyika Ukumbi wa Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar.
Akilimali
pamoja na wazee wenzake na mwakilishi wa baraza la vijana (Makele) walisema
watu hao ni wahuni na wameandikisha majina na wanachama waliofariki na
kuorodhesha kadi zao kujifanya wanapinaga Manji kuongezwa muda.
Akilimali
amesema jambpo hilo litachunguzwa na ikibainika kuwa ni kweli kuna wanachama
waliokufa kwenye wanachama walioorodheshwa waliopeleka barua hiyo wakibainika
watafutwa uanachama.
0 COMMENTS:
Post a Comment