“UKIANGALIA
hivi sasa wanachama wapo mbali sana na klabu yao, kikubwa nitakachoanza nacho
ni kuhakikisha ninaiweka klabu pamoja na wanachama wake.
“Nitafanya
hayo kwa kushirikiana na wenzangu katika baadhi ya mambo, ikiwemo suala la
wanachama kuhakikisha wanashirikishwa katika kuichangia timu yao kwa njia
mbalimbali,” hizo ni kauli za mgombea wa nafasi wa ujumbe katika Klabu ya
Simba, Collin Frisch.
Collins
licha ya kuwa hana jina kubwa kwenye medani ya soka nchini lakini ni mmoja wa
waanzilishi wa Kundi la Friends of Simba ambalo limekuwa karibu na klabu hiyo
na kushiriki katika shughuli nyingi za klabu.
Frisch
anasema, kabla ya kuchukua uamuzi wa kugombea ujumbe Simba, wito mwingi
aliupata kutoka kwa matawi mbalimbali ya Simba yaliyokuwa yakimuomba agombee
nafasi kubwa zaidi ya hiyo.
“Mimi sasa
nimejiajiri na ninafanya shughuli zangu za kilimo,” anasema Frisch na
kuendelea: “Naamini huu ndiyo wakati wangu muafaka wa kuwa kiongozi wa Simba
kwa kuwa sina majukumu mengi kama ilivyokuwa awali.
“Unajua siku
zote uchumi wa klabu unatengenezwa na ufadhili wa makampuni mbalimbali, kampuni
zinapenda timu zenye maendeleo na mafanikio.
“Ili uchumi
ukue lazima tutengeneze imani kwa wanachama na wadau wetu wote, lakini hiyo
itaendana na timu kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa na kitaifa.
“Kwa mfano
kipindi ambacho Mohamed Dewji alipoidhamini Simba, timu ilikuwa na mafanikio
mbalimbali ikiwemo kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.”
Firsch
anaongeza kuwa amepanga kuwa mmoja wa watakaoshawishi uongozi utakaoingia
madarakani kuhakikisha wanamiliki mabasi yao kwa ajili ya wanachama wao.
Kocha
Profesheno
“Kitaaluma
mimi ni kocha na nimesoma kozi nyingi za ukocha kupitia TFF na TAFCA, nina
Gredi B ya Preminary.
“Kwa kupitia
taaluma yangu ya ukocha, nimepanga kushiriki katika kutengeneza timu nzuri za
vijana kuanzia U-17,” anasema Frisch ambaye ni mjumbe wa Lions Club
International inayojishughulisha na masuala ya kijamii.
Kamati
alizokuwepo Simba
“Niliwahi
kuwa kwenye Kamati ya Mashindano ya Simba iliyokuwa na wajumbe kama Hassan
Hasanoo, Adam Mgoi, Danny Manembe na Gerald Luqman iliyochaguliwa na Ismail
Aden Rage.
“Niliwahi
pia kuwa kwenye Kamati ya Usajili chini ya Zakaria Hans Pope, kamati haikufanya
vizuri kutokana na kukosa ushirikiano na uongozi wa Rage ambao unamaliza muda
wake.”
0 COMMENTS:
Post a Comment