UCHAGUZI wa Klabu ya Simba, unatarajiwa kufanyika keshokutwa
jijini Dar es Salaam. Kuna wanachama zaidi ya 23 wanawania nafasi mbalimbali ikiwemo
ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ambayo imependekeza mwanamama mmoja.
Jasmini Badal Sudi, ambaye ni mke wa beki wa zamani wa
Simba, Victor Costa, anaeleza maamuzi yake ya kuamua kuwania nafasi ya ujumbe
wa Kamati ya Utendaji ya Simba.
“Mimi nilikuwa Sekretali wa Simba kuanzia mwa 2003
hadi 2011, nina uzoefu mkubwa kufanya kazi ndani ya Simba, nilifanikiwa kutunza
siri nyingi za klabu mfano mikataba yote ya siri na isiyo ya siri nilikuwa nikiichapa
na kutunza wakati wa utawala wa Hassan Dalali (mwenyekiti),” anasema na
kuendelea:
“Nina elimu ya kutosha, nilihitimu sekondari mwaka 2000,
katika Shule ya Sekondari Sumve Girls ya Mwanza, baadaye nikasomea fani ya Clearing
and Forwarding, kwa sasa ni wakala wa Kampuni ya Cann.
“Mimi ndiye niliyechapisha mikataba ya TBL wakati
wanaingia udhamini na klabu ya Simba. Vilevile nilifanya kazi kwa kujitolea kwa
muda wote huo bila ya kulipwa mshahara na wakati mwingine nilifanya kazi katika
mazingira magumu kama kufungiwa ofisi, lakini nilivumilia na kuendelea na kazi hata
nje ya ofisi.
“Nilifanya yote hayo kutokana na mapenzi yangu kwa
klabu. Mume wangu (Victor) amefanya kazi Simba muda mrefu kama ilivyo kwangu.
Hivyo naamini ninao uzoefu wa kutosha.
“Nina mipango mingi ya kuifanyia Simba, lakini nitakayoyapa
kipaumbele ni kuhakikisa narudisha heshima ya timu pamoja na kuunda umoja wa
akina mama. Nitailinda na kuiheshimu katiba ya timu, pia nina mpango wa
kuiendeleza timu ya wanawake ya Simba Queens.”
0 COMMENTS:
Post a Comment