June 27, 2014



Kocha mpya wa Yanga, Marcio na Maximo amesema hana ugomvi wala chuki na kipa Juma Kaseja.
Akizungumza na waandishi makao makuu ya klabu hiyo, Maximo amesema kama tofauti zake na kipa huyo zilikuwa kipindi kile wako Taifa Stars.

“Sasa naanza mambo yangu upya, sina tofauti na Kaseja wala mtu mwingine.
“Nimesikia Chuji ameachwa, lakini kama ningemkuta bado nilikuwa na nafasi ya kufanya naye kazi bila ya matatizo yoyote.
“Kaseja atakuwa na kazi ya kupambana na changamoto zake katika nafasi ya kipa, hali kadhalika kwangu kama kocha.
“Hivyo hakutakuwa na tatizo na ninawaomba watu watuunge mkono, waangalie kazi yetu kwa jicho la kusaidia na si kukosoa tu,” alisema Maximo.
Kocha huyo raia wa Brazil ambaye ameingia mkataba wa miaka miwili na Yanga, ataanza kazi rasmi Jumatatu.
Maximo na Kaseja walikuwa hawaelewani, wakati huo kocha huyo alikuwa akiinoa Taifa Stars na Kaseja akiwa kipa namba moja wa Simba.
Maximo alidiriki kumuita Ally Mustapha ‘Barthez’ aliyekuwa kipa wa pili wa Simba na kumuacha Kaseja aliyedaka mechi zote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic