KAMA utasikia wachambuzi wanazungumzia
timu ipi inaweza kutwaa Kombe la Dunia ambalo linaanza ndani ya siku tatu, ni
nadra kusikia wakikitaka kikosi cha Italia maarufu kama Azzuri.
Italia inaonekana haina kitu, haina
nafasi na si ya kumtisha yoyote, kitu ambacho ni kocha.
Kocha Cesare Prandelli anaonekana
kujiamini sana na kikosi chake cha watu 23, kuliko hata wachambuzi au wengi
wanaopigia hesabu za michuano hiyo mikubwa zaidi ya soka.
Kikosi cha England katika kila idara
kina watu wa kutosha kabisa wanaoweza kukifikisha mbali au kuwashitua wengi.
Achana na masuala ya rekodi kwanza,
kikosi cha sasa kina wachezaji wazoefu na mahiri wenyewe ujuzi mkubwa na
michuano hiyo, lakini kina vijana ambao wana uwezo mkubwa zaidi.
Kila mmoja ana hamu ya kumuona Mario
Balotelli, kweli ana nafasi ya kung’ara lakini wakongwe kama kipa Gianluigi Buffon, Andrea
Pirlo, Daniele De Rossi, Alberto Aquilani, Thiago Motta na Antonio Cassano
wanajua nini cha kufanya.
Mfano mzuri ni ile Italia ya mwaka
2006 ambayo ilitwaa Kombe la Dunia wakati ilionekana kama haikuwa na nafasi
kabisa.
Ikiongozwa na Fabio Cannavaro
ikapangua miamba mmoja baada ya mwingine hadi ilipotwaa kombe.
Mwaka 2006 nchini Ujerumani haikuwa
bahati kwa Italia, uwezo na uzoefu mkubwa wa wachezaji wake katika michuano ya
kimataifa, wengine bado wanacheza hadi sasa kwenye kikosi hicho.
Lakini angalia vijana wenye umri wa
kati kama kiungo Claudio Marchisio mwenye miaka 28, uwezo wake uko juu sana
kama ilivyo kwa Gabriel Paletta, huyu ni Muitalia mwenye asili ya Argentina
anayekipiga Roma na miaka yake ni 28 pia, lakini fundi kweli.
Kwa washambuliaji, hakuna ubishi kwa
Balotelli, akitulia atakuwa gumzo lakini wafuatilie Ciro Immobile na Lorenzo
Insigne, wana nafasi ya kutikisa.
Italia iko kundi D, lenye timu za
Uruguay, Costa Rica na England, hakika si kundi lahisi hata kidogo.
Iwapo watafanikiwa kutoka hapo,
inawezekana watakamitiwa nusu fainali, fainali au wakiwa na kombe mkononi.
KIKOSI:
Makipa: Gianluigi Buffon
(Juventus), Mattia Perin (Genoa), Salvatore Sirigu (Paris Saint-Germain).
Walinzi: Ignazio Abate (Milan),
Andrea Barzagli (Juventus), Leonardo Bonucci (Juventus), Giorgio Chiellini
(Juventus), Matteo Darmian (Torino), Mattia De Sciglio (Milan), Gabriel Paletta
(Parma).
Viungo: Alberto Aquilani
(Fiorentina), Antonio Candreva (Lazio), Daniele De Rossi (Roma), Claudio
Marchisio (Juventus), Marco Parolo (Parma), Andrea Pirlo (Juventus), Thiago
Motta (Paris Saint-Germain), Marco Verratti (Paris Saint-Germain)
Washambuliaji: Mario Balotelli
(Milan), Antonio Cassano (Parma), Alessio Cerci (Torino), Ciro Immobile (Torino),
Lorenzo Insigne (Napoli).
0 COMMENTS:
Post a Comment