June 25, 2014

LOW

HUENDA mapinduzi yameanza baada ya Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa kupata nafasi ya kuinoa Shaolah FC ya Saudi Arabia akiwa kocha msaidizi.
Mkwasa amewaambia Watanzania kuwa akifanikiwa yeye, ni njia kwa Watanzania wengine. Kweli Tanzania haina makocha wanaotoka nje kufanya kazi kama ilivyo kwa Waganda na Wakenya ambao wamethubutu hata kufanya hapa nyumbani.

Achana na hilo kwanza, katika makocha wakuu 32 waliosafiri hadi Brazil wakiwa na timu zao kwenda kupambana ili kutwaa Kombe la Dunia, Waafrika ni wawili tu.

Huenda hii ni changamoto kwa Afrika kama ile ya Tanzania, Kocha wa Nigeria, Steven Keshi na yule wa Ghana, James Kwesi Appiah ndiyo pekee kutoka bara hili, waliobaki wanatokea katika mabara mengine hasa Ulaya na Amerika Kusini.
KLINSMAN
Ujerumani inaongoza kwa kuwa na walimu hao wa mpira walio katika Kombe la Dunia, imepeleka wanne ambao wanazinoa timu nne tofauti.

Inafuatiwa na nchi tatu za Argentina, Colombia na Italia ambazo zina makocha wanne kila moja, ikiwa na maana timu hizo tatu zina makocha tisa katika michuano hiyo.
KESHI

Nchi nyingine zilizobaki zina makocha wawili ambazo ni Bosnia and Herzegovina na Ufaransa, zilizobaki ni kocha mmojammoja, moja wapo ni Brazil.
APPHIAH

Huu ni mfano wa ile hesabu kwamba makocha kutoka Brazil wamekuwa si kivutio kwa timu nyingi duniani, badala yake wachezaji na soka la nchi hiyo ndiyo linalovuta zaidi.

4:
Ujerumani: Volker Finke (Cameroon), Ottmar Hitzfeld (Uswiss), Jurgen Klinsmann (Marekani), Joachim Low.
3:

Argentina: Jose Pekerman (Colombia), Alejandro Sabella (Argentina), Jorge Sampaoli (Chile).
Colombia: Jorge Luis Pinto (Costa Rica), Reinaldo Rueda (Ecuador), Luis Fernando Suarez  (Honduras).

Italia: Fabio Capello (Urusi), Cesare Prandelli (Italia), Alberto Zaccheroni (Japan).

Ureno: Paul Bento (Ureno), Carlos Queiroz (Iran), Fernando Santos (Ugiriki).

2:
Bosnia and Herzegovina: Vahid Halilhodžić (Algeria), Safet Susic (Bosnia).
Ufaransa: Didier Deschamps, Sabri Lamouchi (Ivory Coast).

1:
Australia: Ange Postecoglou
Ubelgiji: Marc Wilmots
Croatia: Niko Kovač
England: Roy Hodgson
Uholanzi: Luis van Gaal
Nigeria: Steven Keshi
Uruguay: Oscar Tabarez



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic