Uhusiano kati ya mshambuliaji Emmanuel Okwi na uongozi
wa Yanga umebaki asilimia 20 tu.
Yanga
wanaonyesha kutoridhishwa na tabia za Okwi na viongozi waliokutana wanaona bora
aende zake.
Habari za
uhakika kutoka kwa rafiki wa Okwi zinaeleza Yanga imeishamdokeza kuwa inataka
kuvunja mkataba.
Pia imempa masharti
Okwi ambayo akiyatimiza, bado tena suala lake litafikiriwa.
“Kweli hata
OKwi anajua, kaniambia uongozi Yanga unaonekana kama haumhitaji maana umemtupia
lawama nyingi.
“Moja ni
kutocheza mechi za mwisho zikiwemo za Simba na Azam FC kwa madai alipwe fedha
zake, wakati hata yeye hakucheza mechi sita za mwanzo na lilikuwa ni kosa lake.
“Okwi atakutana
na mwanasheria wake kwa mara ya pili na kulijadili suala hilo, hivyo
ikiwezekana akubali kuvunja mkataba,” kilieleza chanzo kutoka Uganda.
Lakini taarifa nyingine
kutoka ndani ya Yanga zilieleza, tayari mchakato wa kumtafuta mrithi wake
umeanza kama lilivyoripoti gazeti hili siku chache zilizopita.
Okwi ambaye ni
mshambuliaji wa zamani wa Simba amekuwa gumzo, lakini msimu uliopita alishindwa
kuwa msaada kwa Yanga ambayo ilimsajili kwa dola 100,000 (Sh milioni 160),
lakini ikamlipa nusu na hapo ndiyo hali ya kutoelewana na kusiganailipoanzia.
0 COMMENTS:
Post a Comment