WAMBURA |
Rais
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, ameruka kwamba Michael
Wambura ambaye ni mgombea wa urais Simba aliyeondolewa kwa mara ya pili, hakuwa
meneja wa kampeni zake wakati akiwania kuingia TFF.
Hali
imekuwa ngumu na wanachama wa Simba wamemcharukia Malinzi kwamba anaiandama
Simba, hasa kutokana na uamuzi wake wa kusitisha uchaguzi uliopangwa kufanyika
Juni 29.
“Jamani mimi sijawahi kutangaza kampeni
meneja, nashangaa watu wanasema kuhusiana na huyu bwana (Wambura).
“Kwanza
mimi sipendi kutaja majina ya watu, pia ninachopenda ni kuona haki inatendeka,”
alisema Malinzi bila ya kusema vipi au wapi haki haijatendeka.
Katika
kampeni zake za uchaguzi, hata siku ya mkutano wake wa kwanza na waandishi
baada ya kushinda urais wa TFF, Wambura alikuwa kati ya watu waliohudhuria kama
rafiki wa karibu wa Malinzi.
Lakini
inaonekana kadiri mambo yanavyozidi kuwa magumu, Malinzi anajaribu kutengeneza
umbali au kumkana Wambura ambaye inajulikana wazi ni rafiki yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment