WANACHAMA WA SIMBA WAKIWA MAKAO MAKUU YA KLABU HIYO HIVI PUNDE WAKIPINGA UAMUZI WA TFF YA MALINZI. |
Mambo
sasa yamekwisha, wanachama wa Simba wamevunja ukimya na kusisitiza wao watapiga
kura za kuchagua viongozi wapya Juni 29 kama ilivyopangwa.
Wanachama
hao bila ya woga wametupa lawana nyingi kwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), kupitia Rais wake, Jamal Malinzi kuwa ni wajanjawajanja na wanataka
kuihujumu Simba.
WANACHAMA HAO WAKIONYESHA KADI ZAO KUSISITIZA WAO SI WABABAISHAJI ILA NI WANACHAMA, TENA HAI. |
Kabla
ya kuzungumza na SALEHJEMBE, wanachama hao walifanya vurugu kubwa wakionyesha
kuwa na hasira kutokana na taarifa za TFF kuusitisha uchaguzi huo hadi iundwe
kama ya maadili.
“Tunapinga,
tunajua Malinzi ni Yanga na anataka kuidhoofisha Simba, hatuwezi kukubaliana na
suala hilo hata kidogo.
“Tunataka
uchaguzi kama kamati ya Ndumbaro ilivyosema. Tutakwenda kupiga kura halafu
tuone sasa, huyu Malinzi anatumiwa na Yanga wenzake,” alisema Ally Mohammed
Said, mmoja wa wanachama na mashabiki waliojitokeza makao makuu ya Simba leo
hii.
Wanachama
hao walikuwa wakiimba nyimbo za kumpinga Malinzi na kusema anataka kuona Simba
haifanyi usajili ili idhoofike na amekuwa na kampeni ya kutaka kuwaingiza
wagombea ambao watafanya kazi pamoja naye na kuidhoofisha Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment