RAGE |
Mwenyekiti wa Simba anayemaliza muda wake, Ismail Aden Rage,
amefunguka na kutoa tamko kali kwa wanachama wa klabu hiyo waliofungua kesi
katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakiomba kusimamishwa kwa Uchaguzi
Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii.
WAMBURA |
Kitendo hicho, kimemfanya mwenyekiti Rage kutoa tamko, ambapo
amewataka wanachama hao kufuta kesi hiyo mara moja kwani kinyume na hapo ni
kuihatarisha klabu kwa ujumla.
Akizungumza na Championi
Jumatano, bosi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini, aliwataka
wanachama hao kupeleka malalamiko yao katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
au mashirikisho ya juu lakini si mahakamani.
“Nimesikia hilo, lakini chondechonde ninawaomba wanachama hao
kama kweli wana mapenzi na Simba kufuta kesi hiyo mara moja, kinyume cha hapo
ni kuiweka pabaya timu.
“Sheria za soka ziko wazi na wanajua kuwa ni hatari masuala
ya soka kupelekwa mahakamani. Niwaombe tu wafute kesi yao mapema na kama
wanaona haki haijatendeka, basi wapeleke malalamiko yao TFF au Caf, lakini si
mahakamani,” alisema Rage.
Wakati huohuo Wambura alipoulizwa kama anahusika alisema: “Masuala
ya wanachama mimi hayanihusu, waulize wenyewe. Mimi sihusiki kwa lolote na tena
mtu asiniulize lolote, waulize wao,”alisema na kukata simu.
SOURCE; CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment