Mwenyekiti wa
Simba, Ismail Aden Rage ametumia busara kuu kwa kumuomba Rais wa TFF, Jamal
Malinzi, uchaguzi ufanyike kama ulivyopangwa.
Rage
amethibitisha kuandika barua hiyo huku akisema uchaguzi ukifanyika Juni 29
itakuwa ahueni kwa Simba.
Rage ambaye ni
Mbunge wa Tabora Mjini amezungumza leo mjini Dodoma na kusema tayari
amewasilisha barua hiyo kwa Malinzi.
“Najua Malinzi
ana madaraka katika hilo, ila vizuri Simba ifanye uchaguzi Juni 29 ili iweze
kumaliza mambo yake mengine.
“Nimemuomba
Malinzi, naomba mnielewe jamani nimemuomba ili asitishe uamuzi wake wa kusogeza
uchaguzi mbele” alisema.
Juzi, Malinzi
alisema amesitisha uchaguzi huo hadi hapo itakapoundwa kamati ya rufaa ndani ya
Simba, kitu ambacho siku iliyofuata kilipingwa na kamati ya uchaguzi,
iliyosisitiza uchaguzi uko palepale Juni 29.
Lakini jana
usiku kukawa na taarifa Rage anataka kuvunja kamati ya uchaguzi.
Alipozungumza
leo akasisitiza: “Kamati ya utendaji imemaliza muda wake, hivyo haiwezi kufanya
kazi ya kuteua kamati ya maadili.”
Wanachama wa
Simba, walimuonya Rage leo asubuhi asiungane na Malinzi na kubadili tarehe ya
uchaguzi, kitu ambacho anaonekana kutumia busara na kuwasilikiliza.
0 COMMENTS:
Post a Comment