HANS POPPE |
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Poppe, ameeleza kuwa wanatarajia
kuwasajili wachezaji wa kimataifa raia wa Kenya na Uganda ambao watatua hapa
nchini keshokutwa Ijumaa.
Hadi
sasa Simba imeshafanikiwa kunasa saini za wachezaji wawili kwa ajili ya msimu
ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambao ni Joram Nassoro aliyetokea Lipuli na
Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ aliyekuwa Kagera Sugar.
Hans Poppe amefunguka kuwa, wanahitaji kufanya usajili
makini kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu kwa kuanza na usajili wa ndani kwa
kuziba mapengo yaliyojitokeza ili waweze kuwa na kikosi bora msimu ujao.
“Tunahitaji
kuboresha kikosi, tayari tumeshasajili wachezaji wawili na leo tunatarajia
kuwasajili wengine wawili kwani mkakati wetu ni kupata wachezaji bora.
“Tunatarajia
kuwasajili wachezaji wawili wa kigeni, mmoja anatokea Kenya na mwingine Uganda
na wanatarajiwa kutua nchini siku ya Ijumaa tayari kwa kuingia nao mkataba mpya
ili waweze kusaidiana na wachezaji waliobakia.
“Tunaanza
na kuwasajili wachezaji wa ndani, kisha tunasajili wachezaji wa nje na mchakato
wa kusaka wachezaji zaidi unaendelea,” alisema Hans Poppe.
Tayari
Simba imeachana na beki wa kati, Mrundi, Gilbert Kaze huku Joseph Owino akidai
hataweza kurudi kwa kuwa amepata timu nyingine.
0 COMMENTS:
Post a Comment