June 17, 2014




Wanachama wa Simba walio katika makao makuu ya klabu hiyo wamemuonyesha Mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage.
Wanachama hao wamesema kumekuwa na taarifa kuwa Rage anataka aivunje kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo.


Wakizungumza na SALEHJEMBE, wanachama hao wamesisitiza kuwa Rage akifanya hivyo ataingia katika kundi la wale wanaoivuruga Simba.

“Wanataka kuivuruga Simba, umeona tatizo hili. Tumesikia mwenyekiti anataka avunje kamati.
“Sasa anaivunja vipi kamati ya uchaguzi, kwani tatizo ni lipi, Simba inataka viongozi tuendelee mbele,” alisema Mohammed Hamis.
Naye Aisha Said amesema hivi: “Tunaona kama kuna njama za kutuvuruga, Rage muda wake umeisha, atuache tuchague viongozi waliopo.
“Si lazima Wambura, naona Simba inataka kusimamisha kila kitu kwa sababu ya mtu mmoja tu, hatuwezi kukubali hili jambo.”
Jana wanachama hao walifurika kwenye makao makuu barabara ya Msimbazi na kupinga uamuzi wa Rais wa TFF, Jamal Malinzi kusogeza uchaguzi.
Lakini wakaungana na kamati ya uchaguzi ambayo ilisisitiza uchaguzi uko palepale kama ulivyopangwa.
Lakini leo kumekuwa na taarifa kwamba, Rage ana mpango wa kutangaza kuivunja kamati ya uchaguzi ambayo inaonekana kushikilia msimamo wa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa wakati yaani Juni 29 kwa manufaa ya Simba ambayo inahitaji kufanya usajili na kuiandaa timu.

6 COMMENTS:

  1. Salah Jembe umekuwa mpiga debe wa tawi la mpila pesa acha kudanganya watu, unafikiri wanacham wa makao makuu hatuwajui? acha uongo kama umepewa chochote poa lakini kuivuruka Simba hamuwezi na hiyo nia ya kuturetea wezi Club ya Simba hatutaki, watawahonga sana ila hawata fanikiwa mwaka huu, magorofani mwisho wao ni 2014 tu, watafute biashara zingine za kuwaingizia kipato sio jezi za Simba , Gazeti na Jengo pamoja na mapato ya milangoni, nyinyi mnao jifanya mnajua sana kuchambua michezo kesho utashangaa Mbeya City wanauza jezi zao Simba na Yanga wamelala leo mnatumika inauma sana, kaeni mbali na Simba.

    ReplyDelete
  2. Acha upuuzi wako wewe, Saleh anatumika kivp? au wewe ndo unatumika? Wezi kina nani? mbona mnadandia mabo hovyohovyo tu, mnasema wezi lakini wanapotoa pesa zao kusaidia timu pindi uongozi unapokuwa umeitelekeza mnakaa kimyaaaaa! ushindi ukipatikana tunashangilia wote, nyie watu cjui namna gani, hivi mnaijua SSC au mnabebeshwa maneno. Kweli kuna mwanachama wa SSC ambae hajui jinsi ambavyo FoS wanavyoisaidia timu mara nyingi inapokuwa imetelekezwa na UONGOZI? Mbona MAZURI yao hamyasemi ambayo ni mengi kuliko hayo MAJUNGU yenu, mnafikiri Wambura atafanya nini SSC. Ebu ondoa upuuzi wako. FoS ni watu wenye heshima zao na wenye shughuli za kueleweka hapa mjini kuliko huyo WAMBURA wenu. Mnajua kila kitu lakini mnajitoa ufahamu. Cresentius Magori au Hans Pope aibe nini SSC zaidi ya kuchangia. Mbona mnakuwa warahisi kudanganywa nyie watu. Kwahyo mnataka waandishi wamsifie mtu wenu sifa ambazo HANA.

    ReplyDelete
  3. duh! si wanatoa kuisadia simba sema wanako[pesha kwa riba maana wanapokuja chukua wanachukua na cha juu, wangekuwa wanasaidia simba si ingekuwa na pesa nyingi sana. mwe mnaelewa maana ya kusaidia na kukopesha kwa riba

    ReplyDelete
  4. Ndambaro is just a messenger who is the boss? friends of Simba.

    ReplyDelete
  5. doctorate wa media law...si alachemsa tazara...dalali wa wachezaji..ameuza wacheaji wangapi ulaya?

    ReplyDelete
  6. BORA AMEACHA UWAKALA....WAKALA UKIUZA MCHEZAJI HALAFU AKARUDI TZ KISA ETI HAJALIPWA, UNATAA WAKALA AFANYE NINI? NDUMBALO YUKO SAHIHI,KAMA HAMJUI KANUNI,KAENI KIMYA NDUMBALO AWANYOSHE.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic