Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe,
ameshindwa kuhudhuria mazoezi ya timu hiyo wikiendi iliyopita kufuatia kufiwa
na shangazi yake aliyefia nchini Rwanda usiku wa kuamkia Jumamosi.
Kocha
Msaidizi wa Simba, Selemani Matola ambaye pia ni mchambuzi maarufu wa soka katika gazeti la Championi, alisema Tambwe ameshindwa kutua mazoezini
hapo kufuatia kupata taarifa za msiba wa shangazi yake ambapo anatarajia
kuondoka kwenda kuzika.
“Kuna wachezaji kadhaa hawajaja kufanya
mazoezi kufuatia matatizo mbalimbali ya kifamilia, Tambwe amepata msiba wa
kufiwa na shangazi yake aliyekuwa akiishi Rwanda ambapo haijajulikana atazikiwa
wapi.
“Iwapo wataamua kuzika Burundi basi na yeye
atakwenda kuzika na kwa sasa anafanya utaratibu wa kujua mazishi yatafanyika
wapi na iwapo itakuwa Rwanda basi hatakwenda,” alisema Matola.
Alipotafutwa Tambwe kuzungumzia suala hilo,
alieleza kuwa bado hajafanya maamuzi ya nini cha kufanya hadi hapo atakapoamua.
0 COMMENTS:
Post a Comment