MASAU BWIRE |
Uongozi wa Ruvu Shooting ya mkoani
Pwani, umesema kuwa mchezo wao ujao wa kirafiki wanaotarajia kucheza Alhamisi
katika Uwanja wa Chamazi dhidi ya Azam utakuwa ni kipimo tosha kwa timu yao.
Ofisa habari wa klabu hiyo, Masau Bwire,
alisema kutokana na Azam kuwa mabingwa watetezi, ndiyo maana wameamua kuomba
kucheza nao mapema.
“Azam ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu
Bara na sisi tumeamua kucheza nao mapema ili waweze kukipima kikosi chetu
ambacho baada ya kufanya mazoezi ya kutosha, tumeona kimeshakuwa tayari kwa
michezo ya Ligi Kuu Bara.
“Tumedhamiria kupata mechi mbili
katika kila wiki mpaka itakapofika wiki moja kabla ya siku ya kuanza ligi kuu
ambapo hapo awali ilikuwa ni Agosti 24 lakini TFF wakaamua kuipeleka hadi
Septemba 20,” alisema Bwire.
Mpaka sasa Ruvu Shooting wameshacheza
mchezo mmoja dhidi ya African Lyona katika Uwanja wa Mabatini, Pwani na kuibuka
na ushindi wa mabao 4-0 huku kocha mkuu wa klabu hiyo, Tom Olaba akikisifia
kikosi chake kutokana na soka safi kilicholionyesha siku hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment