Timu ya JKT
Ruvu imefanikiwa kumnasa aliyekuwa kipa
wa Yanga wa zamani Benjamin Haule kwa kumpatia mkataba wa mwaka mmoja wa kuweza kuitumikia klabu
hiyo kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kipa huyo
aliwahi kuitumikia klabu ya Yanga kipindi cha nyuma, msimu uliomalizika alikuwa
akiitumikia timu ya Ruvu Shooting ambayo pia ni ya ligi kuu.
Katibu wa timu hiyo, David Ngaga,
alisema kuwa wamewasajili wachezaji kadhaa akiwemo kipa Benjamin Haule
ilikuweza kuongeza nguvu katika kikosi chao.
“Ni kweli tumefanikiwa kumsajili kipa
Benjamin Haule kwa ajili ya kuitumikia timu yetu msimu ujao, tumempa mkataba wa
mwaka mmoja kwa mwaka mmoja pamoja
na wachezaji wengine kama kiungo Mohamed Faki (Ashanti United), Ambrose Morris,
Issa Kanduru (Mgambo JKT) Napo Zuberi na Nurdin Mohamed wote JKT Oljoro, hawa
kwa miaka mitatu kwa sababu ni askari,”alisema Ngaga.
0 COMMENTS:
Post a Comment