Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko
Logarusic, ameamua kumuangalia zaidi kiungo wake, Uhuru Selemani
kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Loga ametaka kuona zaidi kiwango chake kabla ya kutoa ruhusa kuwa asajiliwe au la.
Usajili tayari umeongezewa muda kwa siku 14 na Uhuru itabidi achakarike hasa.
"Kama viongozi tumemshauri kocha tumuongezee
mkataba mpya Uhuru ili abaki kuendelea kuichezea Simba, hiyo ni kutokana
kumkosa kiungo mshambuliaji wa Mbeya City, Kaseke (Deus)," kilieleza chanzo.
“Hivyo kocha ameomba muda kwa ajili ya
kumuangalia Uhuru uwezo wake ndani ya uwanja kabla ya kumuongezea mkataba mpya,”kilisema
chanzo hicho.
Alipoulizwa Logarusic kuhusiana na taarifa
hizo alisema: "Wapo wachezaji wengi ninaendelea kuwangalia katika mazoezi yangu
akiwemo Uhuru na yeyote atakayenishawishi nitampa mkataba.
“Bado tuna nafasi za usajili wa wachezaji wa
nyumbani kwa ajili ya msimu ujao, nafasi za profesheno zipo mbili ambazo tayari
tumetoa mapendekezo ya wachezaji wa kuwasajili kwa ajili ya msimu ujao,”alisema
Logarusic.
0 COMMENTS:
Post a Comment