Real Madrid imempoteza mchezaji wake gwiji kuliko
wote, Alfredo di Stefano ambaye amefariki leo mchana.
Ghafla alipata maumivu makali ya moyo akiwa barabarani
karibu kabisa na Uwanja wa Santiago Bernabeu unaomilikiwa na Real Madrid.
Ni msiba mkubwa kwa Madrid kutokana na ukubwa wa di
Stefano katika klabu hiyo ambayo ilimpa urais wa heshima.
Di Stefano anaaminika ndiyo mchezaji mwenye mafaniko makubwa zaidi akiwa na Real Madrid, ameiongoza timu hiyo kutwaa makombe manane ya La Liga, moja la Copa del Rey na matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lakini pia alicheza River Plate ya kwao Argentina na Millonarios ya Colombia na kila nchi amewahi kubeba ubingwa.
MAKOMBE:
REAL MADRID:
-Ligi ya Mabingwa Ulaya (sasa) (Real
Madrid, 1956, 1957, 1958, 1959, 1960)
- Intercontinental
Cup (Real Madrid, 1960)
RIVER PLATE
-
- One
America cup (River Plate, 1947)
REAL MADRID
- Ubingwa wa La Liga (Real Madrid,
1954, 1955, 1957, 1958, 1961, 1962, 1963, 1964)
-Copa del Rey (Real Madrid, 1962)
- Ubingwa wa Argentina (River Plate,
1945, 1947)
MILLONARIOS
-Ubingwa wa Ligi Kuu Colombia (Millonarios
Bogotá, 1949, 1951, 1952, 1953)
0 COMMENTS:
Post a Comment