July 23, 2014

MUSOTI AKIWA NA VIONGOZI WA ZAMANI WA SIMBA, MTAWALA NA MZEE KINESI


Beki kisiki wa Simbam, Donald Musoti, ameungana na kocha Zdravko Logarusic kuwa aongezwe beki mwingine mzoefu wa kati.


Loga alipendekeza hilo katika ripoti yake na kusisitiza Simba inahitaji beki mzoefu mmoja.

Musoti alisajiliwa na Simba msimu uliopita ambapo amekuwa na msaada mkubwa kwa timu hiyo tangu alipojiunga nayo.

Beki huyo Mkenya alisema klabu kubwa kama ya Simba haistahili kuwa na mchezaji mmoja tegemezi katika nafasi moja na badala yake uongozi ungesajili wachezaji zaidi ya mmoja katika nafasi moja ili kuleta ushindani.

“Unajua klabu kubwa kama ya Simba haipaswi kuwa na mchezaji mmoja wa kutegemewa katika namba moja na badala yake kuwe na wachezaji wawili ama watatu ili kusaidiana, wakifanya hivyo timu ndiyo ninapokuwa na ushindani.

“Mfano mzuri msimu uliopita timu ilishindwa kuwa katika kiwango kizuri sababu kubwa ikiwa ni hiyo, ilikuwa akikosekana mtu basi timu inayumba na kushindwa kucheza kama inavyotakiwa.

“Iliniuma kumaliza katika nafasi ya nne kwa timu kubwa kama Simba  ni vyema tukajipanga upya kwa msimu ujao,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic