Mshambuliaji nyota wa Yanga, Mrisho Ngassa amesemaTaifa Stars ina kazi kubwa dhidi ya
Msumbiji lakini akaonyesha kujiamini na kuwaamini wenzake.
“Itakua
kazi ngumu wakati tunarudiana na Msumbiji kwa kuwa mechi ya kwanza imeisha kwa
sare.
“Lakini
tutapambana hadi mwisho, tunaamini tutasonga mbele, tuungeni mkono,” alisema
Ngassa.
Stars
inarudiana na Mambaz wakiwa kwao Maputo katika mechi itakayopigwa wiki ijayo kuwania
kucheza hatua ya makundi kutafuta nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa Afrika.
Mechi
ya kwanza ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.








0 COMMENTS:
Post a Comment