TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA KLABU YA YANGA.
1. Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans Sports Club (YANGA) kwa mamlaka
waliyopewa na Wanachama,kubadilisha, kupunguza au
kuongeza Mjumbe yeyote kwenye Kamati ya Utendaji wakati wowote,kulingana
na changamoto wanazoziona zinazoikabili Klabu ya YANGA, Mwenyekiti na Makamo
Mwenyekiti wa YANGA wanapenda kutoa taarifa rasmi, kuwa Kamati ya Utendaji ya
YANGA na Kamati zote ambazo ziko chini ya Kamati ya Utendaji zitavunjwa kuanzia
tarehe 31 Julai, 2014.
2. Vile vile, Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti
wa YANGA wanapenda kuwashukuru Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya YANGA kwa juhudi zao za
kutekeleza shughuli za Klabu.
3. Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Klabu ya YANGA Bw.Yusuf Manji
na naibu wake Bw.Clement Sanga wanatangaza Kamati ya Utendaji mpya ya Young Africans Sports Club ambayo itakuwa madarakani
kuanzia 1 Agosti, 2014 kama inavyoelezwa
na kila Mjumbe anavyotajwa hapo chini anakuwa na majukumu ya
msingi ya kusimamia kama inavyoonyeshwa pembeni ya
jina lake.
WAJUMBE
WAPYA WA Kamati ya Utendaji ya YANGA ni hawa WAfuaTAO:
1.
Bw.Abubakar Rajabu - Mradi wa Jangwani
City
2.
Bw.Sam Mapande - Sheria na Utawala Bora
3.
Bw.George Fumbuka - Uundwaji wa
Shirika
4.
Bw.Waziri Barnabas - Vibali vya
Hatimiliki na Mahusiano
na
Wafadhili
5. Bw.Abbas Tarimba - Mipango
na Uratibu
6.
Bw.Isaac Chanji na Bw.Seif Ahmed - Uendelezaji
wa Mchezo
7.
Bw.Musa Katabalo - Mauzo ya Bidhaa
8.
Bw.Mohammed Bhinda - Ustawishaji
wa Matawi
9. Bw.David Ndeketela Sekione - Uongezaji wa Wanachama
10.
Bw.Mohammed
Nyenge - Utangazaji wa Habari, Taarifa,
Matangazo n.k.
Wajumbe wa Kamati
ya Utendaji iliyoundwa upya watasimamia kimsingi kamati ndogo zifuatazo:
·
Kamati ya Maadili - Bw.Sam Mapande
·
Kamati ya Nidhamu - Bw.Sam Mapande
·
Kamati ya Uchaguzi - Bw. Sam
Mapande
·
Kamati ya Uchumi na Fedha - Bw.George Fumbuka na Bw.Waziri
Barnabas
·
Kamati ya Mashindano - Bw.Seif Ahmed
& Bw.Isaac Chanji
·
Kamati ya Soka la Vijana na
Wanawake - Bw.Seif Ahmed &Bw.Isaac Chanji
·
Kamati ya
Ufundi - Bw.Seif
Ahmed &Bw.Isaac Chanji
5. Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa YANGA wanamategemeo makubwa kuwa waliotajwa hapo juu watahakikisha wana timiza malengo yaliyokusudiwa na YANGA ili“DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO” mpaka hapo itakapoamuliwa kubadilishwa au kutenguliwa vinginevyo.
6. Mwisho,tunawaomba ushirikiano
wa dhati ili kuhakikisha kuwa YANGA inapiga hatua mbele na inafanikiwa katika kufikia malengo na mipango yake ya maendeleo ya muda mfupi na ya
muda mrefu kwa manufaa ya Klabu, Timu na wana YANGA
popote walipo duniani.
“MUNGU AIBARIKI YANGA.”
(BENO NJOVU)
KATIBU MKUU- YOUNG AFRICANS
SPORTS CLUB
0 COMMENTS:
Post a Comment