July 27, 2014



Yanga inaonyesha imepania kuleta mabadiliko kwa kuingiza damu changa. Kwani katika kamati mpya ya utendaji kuna jina la Sekion David, kiongozi wa kundi la Komedy.

Seki amepewa kazi ya kushughulikia kuongeza wingi wa wanachama katika klabu hiyo. soma chini uone wajumbe wengine wa kamati hiyo ya utendaji.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA KLABU YA YANGA.


1.  Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans Sports Club (YANGA) kwa mamlaka waliyopewa na Wanachama,kubadilisha, kupunguza au kuongeza Mjumbe yeyote kwenye Kamati ya Utendaji wakati wowote,kulingana na changamoto wanazoziona zinazoikabili Klabu ya YANGA, Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa YANGA wanapenda kutoa taarifa rasmi, kuwa Kamati ya Utendaji ya YANGA na Kamati zote ambazo ziko chini ya Kamati ya Utendaji zitavunjwa kuanzia tarehe 31 Julai, 2014.

2.  Vile vile, Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa YANGA wanapenda kuwashukuru Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya YANGA kwa juhudi zao za kutekeleza shughuli za Klabu.

3.  Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Klabu ya YANGA Bw.Yusuf Manji na naibu wake Bw.Clement Sanga wanatangaza Kamati ya Utendaji mpya ya Young Africans Sports Club ambayo itakuwa madarakani kuanzia 1 Agosti, 2014 kama inavyoelezwana kila Mjumbe anavyotajwa hapo chini anakuwa na majukumu ya msingi ya kusimamia kama inavyoonyeshwa pembeni ya jina lake.

WAJUMBE WAPYA WA KAMATI YA UTENDAJI YA YANGA NI HAWA WAFUATAO:

1.  Bw.Abubakar Rajabu                     -       Mradi wa Jangwani City
2.  Bw.Sam Mapande                             Sheria na Utawala Bora
3.  Bw.George Fumbuka                            Uundwaji wa Shirika
4.  Bw.Waziri Barnabas                     -       Vibali vya Hatimiliki na Mahusiano
na Wafadhili
5.  Bw.Abbas Tarimba        Mipango na Uratibu
6.  Bw.Isaac Chanji na Bw.Seif Ahmed       -      Uendelezaji wa Mchezo
7.  Bw.Musa Katabalo                            Mauzo ya Bidhaa
8.  Bw.Mohammed Bhinda                     Ustawishaji wa Matawi
9.  Bw.David Ndeketela Sekione                     Uongezaji wa Wanachama
10.               Bw.Mohammed Nyenge                     Utangazaji wa Habari, Taarifa,
Matangazo n.k.

WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI ILIYOUNDWA UPYA WATASIMAMIA KIMSINGI KAMATI NDOGO ZIFUATAZO:

·              Kamati ya Maadili                     -       Bw.Sam Mapande
·              Kamati ya Nidhamu                     -       Bw.Sam Mapande
·              Kamati ya Uchaguzi                     -       Bw. Sam Mapande
·              Kamati ya Uchumi na  Fedha        -       Bw.George Fumbuka na Bw.Waziri
Barnabas
·              Kamati ya Mashindano              -       Bw.Seif Ahmed &Bw.Isaac Chanji

·              Kamati ya Soka la Vijana na
Wanawake                -    Bw.Seif Ahmed &Bw.Isaac Chanji
·           Kamati ya Ufundi            -    Bw.Seif Ahmed&Bw.Isaac Chanji

5.  Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa YANGA wanamategemeo makubwa kuwa waliotajwa hapo juu watahakikisha wana timiza malengo yaliyokusudiwa naYANGA ili“DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO” mpaka hapo itakapoamuliwa kubadilishwa au kutenguliwa vinginevyo.

6.  Mwisho,tunawaomba ushirikiano wa dhati ili kuhakikishakuwa YANGA inapiga hatua mbele na inafanikiwa katika kufikia malengo na mipango yake ya maendeleo ya muda mfupi na ya muda mrefu kwa manufaa ya Klabu, Timu na wana YANGA popote walipo duniani.

“MUNGU AIBARIKI YANGA.”




(BENO NJOVU)
KATIBU MKUU- YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic