Na Boniface Wambura
Msafara
wa watu 25 wa kikosi cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17
(Serengeti Boys) unaondoka kesho (Julai 28 mwaka huu) kwenda Afrika Kusini kwa
ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos).
Mechi
hiyo ya marudiano ya raundi ya pili itachezwa Jumamosi, Agosti 2 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto, Johannesburg kuanzia saa 9 kamili
mchana kwa saa za Afrika Kusini.
Timu
hizo zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyofanyika Julai 18 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam. Mshindi atacheza
raundi ya mwisho ya michuano hiyo ya Afrika na mshindi wa mechi kati ya Misri
na Congo Brazzaville.
Fainali
za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitafanyika mwakani nchini
Niger.
Wachezaji
wanaounda kikosi cha Serengeti Boys katika msafara huo utakaoondoka saa 2 usiku
kwa ndege ya Fastjet ni Abdallah Jumanne Shimba, Abdulrasul Tahil Bitebo,
Abutwalibu Hamidu Msheri, Adolf Mtsigwa Bitegeko, Ally Aziz Mnasi, Ally Shaban
Mabuyu na Athanas Enemias Mdamu.
Wengine
ni Badru Haji Othman, Baraka Yusuph Baraka, Issa Backy Athuman, Juma Ally
Yusuph, Kelvin Longnus Faru, Martin Kiggi Luseke, Metacha Boniface Mnata,
Mohamed Mussa Abdallah, Omary Ame Omary, Omary Natalis Wayne, Prospal Alloyce
Mushin na Seif Said Seif.
Benchi
la Ufundi linaongozwa na Kocha Mkuu Hababuu Ally Omary akisaidiwa na Stewart
John Hall (Mshauri wa Ufundi), Peter Manyika (Kocha wa makipa), Richard Yomba
(Daktari), na Edward Venance (Mtunza vifaa).
Msafara
wa timu hiyo itakayorejea nyumbani Agosti 4 mwaka huu unaongozwa na mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Khalid
Mohamed Abdallah.
0 COMMENTS:
Post a Comment